Monday, July 30, 2012

TASWA YAPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZOTE ZA CECAFA TANZANIA


TANZANIA SPORTS WRITERS ASSOCIATION (TASWA)
Affiliated to International Sports Press Association (AIPS) & Tanzania Olympic Committee (TOC)
                     
CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), kimesikitishwa na hatua ya Baraza la Michezo la Vyama vya michezo la Afrika Mashariki (CECAFA),  kuwanyanyasa na kuwadhalilisha waandishi wa habari katika mchezo wa fainali Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kufuatia kudhalilishwa huko kwa waandishi katika fainali hiyo ya michuano ya kombe la Kagame kati ya Yanga na Azam, TASWA imelaani kitendo hicho na kuwaondolea utu, udhalilishaji na unyanyasaji kulikosababishwa na baadhi yao kutandikwa makofi na askari polisi mithiri ya vibaka.
Waandishi wa habari za michezo wa Tanzania wamekuwa wasikivu, waadilifu na watu wanaofuata taratibu,  lakini katika fainali hiyo mara baada ya mchezo walifanyiwa vitendo ambavyo havikulingana na tabia yao.
Lengo la waandishi si kuleta vurugu bali kuhakikisha wananchi wanapata habari kwa kila tukio lilikuwa linatokea uwanja, badala yake walionekana hawana thamani mbele ya jamii inayowawakilisha.
TASWA inalaani kitendo cha Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwa kutoa agizo kwa polisi kuwazuia waandishi kuingia uwanjani kumalizia kazi zao za kuhoji makocha na wachezaji, hali iliyosababisha vurugu.
CECAFA walijenga urafiki wa karibu na waandishi kipindi chote cha mashindano hayo na Kagame kwa lengo la kuyatangaza , lakini mwisho wa yote walionekana kama taulo la deki limekuwa na thamini pale ambapo linahitajika kwa deki, lakini baada ya hapo halina thamani tena.
Lakini TASWA inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, kufuatia baadhi ya waandishi kuonesha utovu wa nidhamu kama baadhi ya viongozi wa TFF na CECAFA walivyodai kuwa walionesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kutoa maneno ya kashfa na kutaka kumpiga Musonye
Kufuatia hatua hiyo TASWA imechukua maamuzi yafuatayo
1.Kutoandika jambo lolote linahusu Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki (CECAFA).
2.Kutoandika jambo lolote linahusu mashindano yoyote yaliyo chini ya  CECAFA.
Ili kuweza kufanya kazi pamoja na CECAFA,TASWA inataka kuombwa radhi na CECAFA kutokana na kitendo hicho na kuwalipa fidia waandishi ambao wamepoteza vifaa vya vya kazi na wengine kuhalibiwa vifaa vyao.
TASWA inatoa onyo kali kwa baadhi ya vyama,viongozi na makampuni wenye tabia ya kutotoa ushirikiano na dharau kwa waandishi wanapokuwa kwenye kazi zao.
Juma Abbas Pinto
CHAIRMAN
Julai 30, 2012

No comments:

Post a Comment