Monday, July 2, 2012

NI ZAMA ZA HISPANIA

Nahodha Iker Casillas akinyanyua juu kombe baada ya kuifunga Italia katika fainali kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine usiku wa kuamkia leo.
Nahodha Iker Casillas akinyanyua juu kombe baada ya kuifunga Italia katika fainali kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine usiku wa kuamkia leo.

Nahodha Iker Casillas akinyanyua juu kombe baada ya kuifunga Italia katika fainali kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine usiku wa kuamkia leo.
Xabi Alonso akibeba kombe huku akifurahi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Hispania baada ya kuifunga Italia katika fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa  Olimpiki mjini Kiev, usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS

KIEV, Ukraine
HISPANIA walisiliba nafasi yao kama wababe wa dunia katika soka kwa staili ya aina yake baada ya kuisambaratisha Italia kwa mabao 4-0 na kutetea taji lao la Ulaya usiku wa kuamkia leo.

Ushindi huo katika mechi ya fainali iliyojaa dhamira ya kushambulia, umemaanisha kwamba Hispania wamekuwa timu ya kwanza katika historia kutwaa mataji ya Euro mawili mfululizo huku katikati ya mataji hayo wakibeba Kombe la Dunia 2010.

Hispania walishambulia tangu mwanzo na wakapata goli la kuongoza katika dakika ya 14 kupitia kwa David Silva aliyefunga kwa kichwa kufuatia krosi ya Cesc Fabregas na dakika nne kabla ya mapumziko wakaongeza goli la pili kupitia kwa beki wa kushoto aliyekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Barcelona, Jordi Alba, baada ya kuipita kwa kasi ya umeme safu ya ulinzi iliyokuwa imelala ya Italia akitumia pasi ya "maestro" Xavi Hernandez kabla ya kumtungua kirahisi kipa Gianluigi Buffon. 

Fernando Torres, ambaye alifunga goli la ushindi la Hispania wakati walipotwaa ubingwa katika fainali za Euro zilizopita, alikuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga goli katika mechi mbili za fainali za michuano hiyo wakati alipoongeza la tatu kwa timu yake katika dakika ya 86 na kisha akampikia mtokea benchi mwenzake, Juan Mata, kufunga la nne katika dakika ya 88.

Italia walianza kwa kutawala katika dakika za awali lakini kila walipotarajia kufunga, kipa Iker Casillas alidumisha rekodi yake ya kutoruhusu goli hata moja katika hatua ya mtoano katika mechi 10 mfululizo walizoshinda.

Matumaini ya Italia ya "kurejea mchezoni" yalitoweka wakati mchezaji wa tatu wa akiba aliyeingia Thiago Motta kuumia misuli ya nyuma ya paja na kutoka na kuilazimisha timu yake kucheza wakiwa 10 uwanjani kwa dakika 30 zote za mwisho.

  

No comments:

Post a Comment