Sunday, July 22, 2012

MODRIC KUTOZWA FAINI KWA KUGOMA KUFANYA MAZOEZI AKISHINIKIZA KUONDOKA TOTTENHAM

Luka Modric

LUKA Modric atatozwa faini ya zaidi ya paundi 80,000 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 196) kwa kukataa kufanya mazoezi wakati akishinikiza kuhama kutoka Tottenham Hotspur.

Kiugo huyo mwenye umri wa miaka 26, hata hivyo, anaaminika kuwa amepanda ndege kuelekea Los Angeles jana Jumamosi akiambatana na kikosi cha timu hiyo kilichopaa kwenda Marekani kujiandaa na msimu mpya.

Tottenham haikutoa orodha ya wachezaji waliosafiri na timu, lakini kulikuwa na uvumi kutoka Hispania kwamba mchezaji huyo ametishia kutosafiri.

Modric sasa anatarajiwa kuwasilisha maombi ya kuhamia Real Madrid ingawa Spurs imesisitiza kwamba haitashusha bei ya paundi milioni 40 waliyomuwekea Mcroatia.

Kwa kuwa Spurs imedhamiria kutoshusha bei, mvutano, kama ilivyokuwa katika kipindi kilichopita cha usajili wakati Modric alipotaka kutua Chelsea, unatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa kipindi cha usajili mwisho wa Agosti.

Modric alikataa kufanya mazoezi Ijumaa kabla ya kesho yake timu kupanda ndege, na atapigwa faini ya mshahara wake wa wiki mbili, ambao ni zaidi ya paundi 80,000 jumla, na kocha mpya wa Spurs, Andre Villas-Boas.

No comments:

Post a Comment