Tuesday, July 31, 2012

HAYA HAYA HAYAAAA... ULE MPAMBANO WA MITA 100 OLIMPIKI NI AGOSTI 5

Muunganiko wa picha zinazowaonyesha wanariadha wenye kasi zaidi ambao watachuana katika mbio za mita 100 katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Agosti 5, 2012. Kutoka kushoto mstari wa juu ni Wajamaica Usain Bolt, Asafa Powell and Yohan Blake. Mstari wa katikati kutoka kushoto ni Justin Gatlin na Tyson Gay wa Marekani. Mstari wa chini kutoka kushoto ni Keston Bledman (Trinidad na Tobago), Christophe Lemaitre wa Ufaransa Ryan Bailey wa Marekani. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 116, mbio za Olimpiki za mita 100 zimekuwa zikileta ushindani mkubwa, machungu, utata, fadhaa, maajabu na furaha isiyomithilika - yote hayo yakipatikana katika mbio hizo ambazo humalizika mapema zaidi muda utakaoutumia kutamka neno "Baron Pierre de Coubertin." Picha: REUTERS

No comments:

Post a Comment