Tuesday, July 31, 2012

ALIYEMDUNDA KIDUNDA ANG'ARA TATTOO BORA ZA OLIMPIKI

Mchoro wa ringi za nembo ya Olimpiki zikionekana kwa mwogeleaji wa Marekani, Kathleen Hersey wakati wa mashindano ya Santa Clara International Grand Prix mjini California, Juni 19, 2011. Picha: REUTERS
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiwa hoi baada ya kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 na bondia wa Moldova, Vasilii Belous (kushoto) katika hatua ya 32-Bora uzito wa welter (kg.69) kwenye Ukumbi wa ExCeL katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Julai 29, 2012.
Bondia wa Moldova, Vasilii Belous (kushoto) akionyesha tattoo yake wakati akizichapa dhidi ya bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda, wakati pambano lao la uzito wa welter (kg. 69) hatua ya 32-Bora kwenye Ukumbi wa ExCeL katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Julai 29, 2012. Picha: REUTERS
Mwogeleaji wa Canada akionyesha mchoro wa ringi za nembo ya Olimpiki kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya London 2012 mjini London Julai 27, 2012. REUTERS
Mchoro wa kipepeo wa Vanessa Ferrari wa Italy ukionekana wakati kimwana huyo akidhuhuria mazoezi kwenye ukumbi wa O2 Arena kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Julai 26, 2012. Picha: REUTERS
Khatuna Lorig wa Marekani akichukua mshale akionekana na mchoro wa ndege tai wa Kimarekani wakati wa robo fainali ya mashindano ya kulenga shabaha katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Julai 29, 2012. Picha: REUTERS
Mwogeleaji wa Italia, Ilaria Bianchi akijiandaa kufanta mazoezi kwenye bwawa kuu la Aquatics Centre kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Julai 26, 2012. Picha: REUTERS
Mchoro wa ringi za nembo ya Olimpiki ukionekana mgongoni mwa Marta Pihan-Kulesza wa Poland wakati wa mashindano ya "gymnastics"  kwenye Ukumbi wa North Greenwich Arena wakati wa Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Julai 29, 2012. Picha: REUTERS
Mchezaji wa mpira wa wavu wa timu ya wanaume ya Brazil, Alison akijifua kwa ajili ya mechi ya ufukweni katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 mjini London Julai 26, 2012. Picha: REUTERS
Sarah Poewe wa timu ya taifa ya kuogolea ya Ujerumani akionekana na mchoro wa nembo ya Olimpiki wakati akishiriki mazoezi kabla ya Michezo ya Olimpiki ya London 2012 mjini Hamburg Julai 23, 2012. Picha: REUTERS
Muogeleaji wa Canada akionekana na ringi za nembo Olimpiki kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya London Julai 27, 2012. Picha: REUTERS

No comments:

Post a Comment