Monday, July 2, 2012

AFANDE, AY WAPAGAWISHA TAMASHA LA COCA COLA MWANZA

Msanii wa bongo fleva, Ambwene Yesaya (AY) akipagawisha mashabiki wake wakati wa tamasha la "Sababu Bilioni za Kuithamini Afrika" lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ambalo limefanyika pia katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha linadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi jamii ya Coca Cola kwa lengo la kuibua vipaji vya muziki.

Msanii wa bongofleva Afande Sele akitumbuiza wakati wa tamasha la "Sababu Bilioni za Kuithamini Afrika" lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola kwa lengo la kuibua vipaji.

Wasanii wa vichekesho Kidungandimu na Kobelo wakitoa burudani ya vichekesho wakati wa tamasha la "Sababu Bilioni za Kuithamini Afrika" lililofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca- Cola.

Msanii chipukizi wa bongofleva C-Sir Madini akionyesha umahiri  wa kuimba wakati wa tamasha la "Sababu Bilioni za Kuithamini Afrika" lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ambalo limefanyika pia katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha lilidhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca- Cola kwa lengo la kuibua vipaji vya muziki.  

VIJANA kutoka kona mbalimbali za jiji la Mwanza wamejitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la Coca-Cola lijulikanao kama "Sababu Bilioni Moja za Kuithamni Afrika" likiwa na lengo la kuwahamasisha vijana na wananchi kwa ujumla kujiamini na kuipenda nchi yao na Afrika kwa ujumla.

Tamasha hilo la aina yake liliandaliwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottlers yenye makao yake hapa mjini Mwanza ambapo kivutio kikubwa katika tamasha hilo  kilikuwa ni wasanii wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya Bongo Flava, Ambwene Yesayah  marufu kama AY na Selemani Msindi a.k.a Afande Sele ambao waliwafanya maelfu ya vijana kusukumana huku na kule ili kupata nafasi nzuri ya kuwaona wanamuziki hao machachari wakifanya mambao jukwaani.

Katika tamasha hilo pia baadhi ya wasanii chipukizi walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao walipojimwaga uwanjani kuimba na kucheza pamoja na wasanii hao.

Aidha vijana hao pamoja na kuipongeza kampuni ya Nyanza Bottlers kwa kuona umuhimu wa kuandaa tamasha hilo, wamezitaka kampuni nyingine kuona umuhimu wa kusaidia kuibua vipaji vya vijana.

Kwa upande wao wasanii hao  chipukizi  wa Bongo Flava pamoja na kuipongeza   kampuni ya Coca-Cola kwa  tamasha hilo na mengine yanayoigusa jamii hasa vijana a wameendelea kusema kuwa kampeni hii ya "Sababu Bilioni Moja za Kuithamini Afrika" imekuja wakati mwafaka na itasaidia kuhamisisha uzalendo miongoni mwa vijana.

Akizungumza katika tamasha hilo Meneja Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Alfred Malandu amesema Nyanza Bottlers kupitia kinywaji chake cha Coca-Cola itaendelea kuhamasisha jamii kujivunia na kutumia vitu vinavyopatikana Afrika.

Tamasha hilo pamoja na burudani mbalimbali ikiwemo muziki kulikuwa na michezo mbalimbali kama vile shindano la kupiga danadana.


No comments:

Post a Comment