Thursday, June 28, 2012

RONALDO ASHUTUMIWA PENALTI

Ronaldo (kulia), Pepe (kushoto) na Fabio Coentrao wakiangalia kwa kukata tamaa hatua ya kupigiana "matuta" wakati nusu fainali ya UEFA Euro 2012 dhidi ya Hispania kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ameangushiwa fuko la lawama kwa kutopiga penalti ya mapema na kuisaidia timu yake na badala yake kutaka aje kupiga penalti ya mwisho ili aonekane shujaa wa timu.

Wakati Ureno wakiwa nyuma kwa penalti 3-2, Ronaldo anashutumiwa kutoona umuhimu wa kwenda kupiga penalti iliyofuata ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kushindana na Hispania, lakini akamuachia beki Bruno Alves akapige penalti ya nne huku wakifahamu kwamba kukosa penalti hiyo kungewapa Hispania nafasi ya kusonga mbele endapo wangefunga penalti yao ya nne.

Jambo hilo ndilo lililotokea kwani Alves aligongesha besela na Fabregas akafunga penalti iliyowapa Hispania ushindi wa 4-2 na kumuacha Ronaldo akiwa hajaisaidia timu yake katika hatua hiyo ya kupigiana "matuta".


Hata hivyo, kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Paulo Bento, amemtetea nahodha wake kwa kutopiga penalti ya mapema. 

"Tulipanga kwamba kama matokeo yatakuwa 4-4, Ronaldo apige ya tano kwa sababu angepiga kitofauti. Lakini bahati haikuwa yetu," alisema Bento. 

No comments:

Post a Comment