LEBRON AIPAISHA MIAMI NBA
LeBron James |
MIAMI, Marekani
TIMU ya mpira wa kikapu ya Miami Heat
imeifunga Oklahoma City Thunder kwa pointi 91-85 na kutwaa uongozi wa 2-1
katika mechi ya tatu ya mfululizo wa mechi saba za fainali ya Ligi ya Mpira wa
Kikapu Marekani (NBA) juzi.
LeBron James aliongoza
katika ufungaji baada ya kufunga pointi 29, Dwyane Wade akaongeza nyingine 25
kwa Miami huku nyota wa Oklahoma, Kevin Durant akifunga pia pointi 25. Mechi
yao ya nne itachezwa kesho mjini Miami.
No comments:
Post a Comment