Wednesday, June 27, 2012

MASOMBO LINO AWAPAGAWISHA SIMBA TCC

Masombo Lino (kulia) akimiliki mpira baada ya kumpokonya mpira Kiggi Makasi (kushoto) kama vile alimuazima wakati wa mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Jamaa ni mzuri kwa kweli na Simba watamsahau Yondani.

Na Prince Akbar 
BEKI wa Simba SC, Masombo Lino Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jana alikuwa kivutio kikubwa katika mazoezi ya klabu hiyo, Uwanja wa TCC, Chang’ombe, Dar es Salaam. Katika mazoezi yaliyoongozwa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovick, Masombo alionyesha ni mzuri kwenye kuzuia na kusaidia mashambulizi pia. Mashabiki wa Simba walikuwa wenye furaha kubwa TCC jana kutokana na mavituuz yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wao wengine wapya pia. Mazoezi ya Simba yanaendelea leo kwenye Uwanja huo, kujiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano iliyopangwa kuanza Julai 14 hadi 29, mwakani. Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lilitua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba. Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wamemsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga. 

Chanzo: bongostaz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment