Wednesday, June 27, 2012

SIMBA YATEMA WATANO, MACHAKU KWA MKOPO

Ali Mustapha 'Barthez' akijifua mazoezini Yanga alikohamia.
Gervais Kago
Shija Mkina
Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Simba imeachana na wachezaji watano waliomaliza mikataba yao, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Wachezaji waliomaliza mikataba yao Simba na hawataongezwa kwa mujibu wa klabu hiyo ni Ally Mustafa 'Barthez' aliyetua Yanga, Mganda Derick Walulya, Gervais Kago kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, beki Juma Jabu huku Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu.

Wachezaji ambao Simba inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Salum Machaku, Rajab Isihaka, Haruna Shamte na Shija Mkina.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TFF inayofuatia klabu tano kuwasilisha katika shirikisho hilo majina ya wachezaji inaoachana nao kwa ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa 2012/2013, Azam imewasitishia mikataba wachezaji watatu ambao ni Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino Augustino.

Taarifa hiyo ilisema wachezaji 12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar na ikawataja kuwa ni Cassian Ponera, Hamis Msafiri, Hussein Swedi, Ibrahim Mamba, Martin Muganyizi, Mike Katende, Moses Musome, Msafiri Davo, Said Ahmed, Said Dilunga, Steven Mazanda na Yona Ndabila.

Timu ya Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11.

Wachezaji walioachwa Polisi Morogoro ni Abdul Ibadi, Ally Moshi, Benedict Kitangita, Hassan Kodo, Hussein Lutaweangu, Hussein Sheikh, Juma Maboga, Mafwimbo Lutty, Makungu Slim, Mbaraka Masenga, Method Andrew, Moses Mtitu, Ramadhan Kilumbanga, Ramadhan Toyoyo, Said Kawambwa, Salum Juma na Thobias John.

Tanzania Prisons imewaacha Adam Mtumwa, Dickson Oswald, Exavery Mapunda, Ismail Selemani, Lwitiko Joseph, Mbega Daffa, Mwamba Mkumbwa, Musa Kidodo, Rajab Ally, Richard Mwakalinga na Sweetbert Ajiro.

Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuacha wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu. Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment