Thursday, June 28, 2012

MAKUNDI KOMBE LA KAGAME KUPANGWA KESHO

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye

Na Mwandishi Wetu
HAFLA ya kupanga makundi na ratiba kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame itafanyika kesho (Juni 29, 2012) kwenye ofisi za TFF, taarifa ya shirikisho hilo la soka nchini imesema leo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, hafla hiyo itafanyika kuanzia saa 6:00 mchana.
Michuano ya Klabu Bingwa za Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kagame itaanza Julai 14 ikishirikisha takriban timu 12 za ukanda huu wa CECAFA.

Tanzania bara itawakilishwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, Simba na washindi wa pili Azam, wakati Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo. Walitwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga mahasimu wao Simba katika mechi ya fainali mwaka jana.

No comments:

Post a Comment