Thursday, June 28, 2012

FABREGAS ANA KIZIZI TIMU YA TAIFA HISPANIA

Cesc Fabregas wa Hispania akishangilia baada ya kufunga penalti ya ushindi dhidi ya Ureno baada ya mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.

Cesc Fabregas wa Hispania (kulia) akishangilia na nahodha wake, Iker Casillas baada ya kufunga penalti ya ushindi dhidi ya Ureno baada ya mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.

Cesc Fabregas wa Hispania akifunga penalti ya ushindi dhidi ya kipa Rui PatrĂ­cio wa Ureno wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.

Cesc Fabregas wa Hispania akifunga penalti ya ushindi dhidi ya kipa Rui PatrĂ­cio wa Ureno wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.

MCHEZAJI aliyeingia kutokea benchi Cesc Fabregas ana "kizizi" cha kupika mafanikio pale yanapohitajika kwa timu ya taifa ya Hispania.


Penalti yake ya ushindi dhidi ya Ureno wakati wa kupigiana "matuta" katika mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 jana usiku, iliongeza mkusanyiko wa matukio yake ya kuipa mafanikio Hispania baada ya kupiga pasi ya mwisho iliyozaa bao lililoipa nchi yake ubingwa wao kwanza wa katika historia ya Kombe la Dunia 2010.


Italia pia wataikumbuka penalti yake ya ushindi baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi yao ya robo fainali katika michuano iliyopita ya Euro.


"Nilikuwa na hisia za masihara kuhusu upigaji wa penalti na nilikuwa nazifikiria jioni hii. Kwamba maisha yamenipa fursa nyingine kama hii ni jambo kubwa," Fabregas alisema baada ya ushindi wa Hispania wa 4-2.


"Niliposogea kupiga penalti ile niliuambia mpira kwamba tunataka kuweka historia na haupaswi kuniangusha. Awali waliniambia nikapige penalti ya pili lakini nikasema hapana nipeni ya tano kwa sababu nina bahati."


Kujiamini kwa Fabregas kukathibitisha kulikuwa sahihi zaidi ya imani ya Ureno kumuacha mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aje kupiga penalti ya mwisho.


Mchezaji huyo ghali zaidi duniani alibaki amesimama kama mtu aliyekosa msaada wakati akimshuhudia kiungo wa Barcelona, Fabregas, akizima ndoto za Ureno katika michuano hiyo.



No comments:

Post a Comment