Saturday, June 30, 2012

DIARRA ANAENDA AC MILAN - WAKALA

Mchezaji wa Real Madrid, Lassana Diarra "akila bata" ufukweni Miami, Florida, Marekani.
Mchezaji wa Real Madrid, Lassana Diarra (kulia) akijiachia na washkaji ufukweni Miami, Florida, Marekani.

WAKALA anayeheshimika wa Italia, Enzo Bronzetti anatarajia kiungo wa Real Madrid, Lassana Diarra ajiunge na AC Milan.

Kiungo huyo mwenye Umri wa miaka 27 amekuwa klabuni Real tangu mwaka 2009 alipojiunga akitokea Portsmouth. Amechezea pia klabu kam,a Le Havre, Chelsea na Arsenal.

"Diarra yuko mapumzikoni Marekani hivi sasa," Bronzetti aliliambia gazeti la Hispania la Marca. "Hata hivyo, mara atakaporejea, atasaka maafikiano na Milan."

No comments:

Post a Comment