Saturday, June 30, 2012

BALOTELLI: WATU WANAONEA WIVU MWILI WANGU

Mario Balotelli wa Italia akishangilia baada ya kufunga goli lake la pili wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 dhidi ya Ujerumani kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, Poland Juni 28, 2012.

Mario Balotelli wa Italia (kulia) akishangilia baada ya kufunga goli lake la pili wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 dhidi ya Ujerumani kwenye Uwanja wa Taifa mjini Warsaw, Poland Juni 28, 2012.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli ametetea staili yake ya kushangilia dhidi ya Ujerumani.

Balotelli alifua shati lake baada ya kufunga goli lake la pili dhidi ya Ujerumani lakini hakudokeza namna atakavyoshangilia ushindi ama goli dhidi ya Hispania katika fainali ya Euro kesho.

Balotelli alisema: "Sina cha kusema kuhusu namna nilivyoshangilia goli langu la pili.

"Mliona. Mnaweza kuhukumu. Kuna mtu alichukizwa na jinsi nilivyoshangilia goli langu la pilu?

"Kwa sababu waliona mwili wangu na wana wivu.

"Hata hivyo, sina namna maalum ya kushangilia kwenye fainali. Mimi hudumisha matumaini kwamba nitafunga. Nafikiria kufunga tu — sifikirii kuhusu kushangilia."

No comments:

Post a Comment