Wednesday, June 27, 2012

DIAKITE ASAINI MKATABA WA KUDUMU QPR

Samba Diakite wa QPR (katikati) akimtoka beki wa Tottenham, Benoit Assou-Ekotto (kushoto) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Loftus Road mjini London, England Aprili 21, 2012.

LONDON, Uingereza
KIUNGO wa Mali, Samba Diakite amesaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Queens Park Rangers baada ya awali kujiunga na klabu hiyo klwa mkopo msimu uliopita, klabu hiyo ya ligi kuu ya England ilisema jana.

Diakite, 23, aliichezea QPR mara tisa msimu uliopita kufuatia uhamisho wake wa mkopo akitokea Nancy ya Ligi Kuu ya Ufaransa mwezi Januari.

"Samba alikuwa mtu sahihi tuliyempata Januari, hivyo tumefurahi kwamba amejiunga nasi jumla," kocha wa QPR, Mark Hughes alisema kwenye tovuti ya klabu hiyo (www.qpr.co.uk).

"Ana kasi, ngangari na uwezo wa kumiliki mpira na atakuwa aseti kubwa kwetu."

QPR ilimaliza katika nafasi ya 17 msimu uliopita, pointi moja juu ya ukanda wa kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment