Tuesday, October 1, 2013

REDD'S MISS TANZANIA ALIPOTEMBELEA TBL

Redd’s Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TBL Robin Goestzche na kushoto ni Mkugenzi wa Masoko wa TBL, Kushila Thomas. Wa pili kushoto ni mshindi wa pili wa Redd’s Miss Tanzania 2013, Latifa Mohamed na wa pili kulia ni mshindi wa tatu, Clara Bayo.
 

Meneja Masoko wa TBL nchini, Fimbo Butallah (kulia) akimpongeza mshindi wa shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa mara baada ya kukamilisha mazungumzo ya utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL nchini Tanzania, Robin Goestzche.

Redd’s Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa katikati akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa kampuni ya bia nchini (TBL).

Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tanzania kwa mkurugenzi mkuu wa TBL, Robin Goestzche (kulia).

Mkurugenzi Mkuu wa TBL nchini Tanzania, Robin Goestzche akimpongeza Redd’s Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa na kushoto ni Mkugenzi wa Masoko wa TBL Kushila Thomas.
 

Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tanzania kwa mkurugenzi mkuu wa TBL, Robin Goestzche (kulia).


REDD’S Miss Tanzania, Happiness Watimanywa jana alitembelea rasmi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) walio wadhamini wa shindano hilo, ambapo alikutana na uongozi wa juu ili kujitambulisha.

Katika ziara hiyo, Happiness alifuatana na mshindi wa pili, Latifa Mohammed, mshindi wa tatu, Clara Bayo pamoja na Kamati ya Redd’s Miss Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukutana na mrembo huyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goestache alisema, wao kama wadhamini wakuu wanajisifu kuwa sehemu ya mafanikio ya Redd’s Miss Tanzania, huku akimsifu mrembo huyo kwa ushindi wake.

“Kila mmoja kati yetu anajua shindano lilivyokuwa gumu, warembo wote walikuwa na sifa na ninawapongeza ninyi mlioshinda na tunawakaribisha katika familia ya TBL,” alisema.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushillah Thomas, naye alitumia fursa hiyo kuwapongeza warembo hao na kusema ana imani kubwa nao watafanya vizuri zaidi katika kipindi chao.

Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema, toka waanze kudhamini shindano hilo wamepata mafanikio makubwa mno, huku kukiwa na kazi nyingi za jamii wanazozifanya na warembo waliofanikiwa kutwaa taji hilo.

Happiness naye aliishukuru TBL kwa kudhamini shindano hilo na kusema anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya familia ya Redd’s.

“Kwa kiasi kikubwa nawashukuru kutokana na kudhamini shindano hili kwa muda wa miaka 13, kwani mmesaidia mengi kwa warembo na najivunia kuvaa sura ya Redd’s.”

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment