Friday, August 23, 2013

NEYMAR AFURAHIA GOLI LA KWANZA

Neymar (wa pili kulia) wa Barcelona akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Atletico de Madrid wakati wa mechi yao ya kwanza ya Supa Copa kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania Agosti 21, 2013.
Neymar wa Barcelona akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Atletico de Madrid wakati wa mechi yao ya kwanza ya Supa Copa kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania Agosti 21, 2013.

Neymar (wa pili kushoto) wa Barcelona akishinda kuruka Juan Francisco Torres 'Juanfran' na kufunga goli dhidi ya kipa wa Atletico de Madrid, Thibaut Courtois (kulia) wakati wa mechi yao ya kwanza ya Supa Copa kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania Agosti 21, 2013.
Neymar (wa pili kulia) wa Barcelona akifunga goli dhidi ya kipa wa Atletico de Madrid, Thibaut Courtois (kulia) wakati wa mechi yao ya kwanza ya Supa Copa kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania Agosti 21, 2013.

NEYMAR ameelezea furaha yake kufunga goli lake la kwanza la kimashindano tangu ajiunge na Barcelona katika sare yao ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mechi yao ya kwanza ya Supa Copa.

Mbrazil huyo aliingia kutokea benchi Jumatano na kufunga goli la kusawazisha baada ya nyota wa zamani wa Barca, David Villa kuifungia timu yake mpya goli la kuongoza.

"Nina furaha kwamba nilifunga goli la kusawazisha. Ilikuwa ni mechi ngumu dhidi ya wachezaji bora,” alisema.

"Atletico ni timu kubwa, na wameonyesha tena katika mechi hii. Ni matokeomazuri na sasa tunapaswa kumaliza kazi nyumbani."

No comments:

Post a Comment