Friday, June 7, 2013

WEMBAMBA WA NEYMAR WAZUA MJADALA

Neymar’s weight situation
Mbavu tupu... Neymar akifanyiwa vipimo kwa ajili ya kujiunga na Barcelona
JUNI 5, 2013 gazeti la Sport liliripoti kwamba Jose Luis Runco, daktari wa viungo wa timu ya taifa ya Brazil, alitoa maoni yake kwamba ingawa umbo la Neymar ni jembamba kwa asili, itamsaidia sana kama ataongeza uzito kidogo. 

Runco alisema madaktari wa FC Barcelona pia walitoa maoni kama hayo. Hasa baada ya kumwambia aruke wakati wa kumfanyia vipimo.

Jose-Luis-Runco
Daktari wa viungo wa timu ya taifa ya Brazil, José Luis Runco
Kwa mujibu wa vipimo vilivyofanyika Barça, Neymar ana urefu wa futi 5 na inchi 9 (ambazo ni sawa na mita 1.75) na ana uzito wa kilo 64.5. 

Runco alikaririwa akisema, "kwa kuwa ameshakikishiwa hatma yake katika timu kama Barcelona, hatashutumiwa sana na atakuwa na wakati mwepesi wa kuongeza kilo mbili ama tatu anazozihitaji."

Alisema pia kuongeza uzito huku kunapaswa kufanywa taratibu kwa mazoezi na mlo ambavyo atapata Barcelona, hivyo jambo hilo halitatokea kwa usiku mmoja.

Tumeshuhudia mabadiliko ya kimwili kwa wanamichezo wenye mafanikio. 

Kwa mfano, Iniesta ana urefu futi 5 na inchi 7 (sawa na mita 1.7) na uzito wa kg 65 ambao ni za mchezaji mwembamba kwa viwango vya soka. 

Iniesta anafanikiwa kwa kutumia vyema ufupi wake (low centre of gravity) na uwezo mkubwa wa miliki mpira. Iniesta mara nyingi amekuwa akicheza vyema kwenye wingi ya kushoto lakini anacheza tofauti na Neymar. 

Nyota mpya wa Barça, Neymar kwa sasa ana uzito takriban sawa na na Iniesta lakini yenye ni mrefu kwa inchi mbili zaidi na staili yake inahitaji kupambana bega kwa bega na wapinzani wake. Iko wazi kwamba kwa mwili wake mwembamba wa sasa, Neymar anahitaji kuongeza nguvu.
CR 2008 vs 2013
Cristiano Ronaldo alivyokuwa mwaka 2008 wakati akiichezea Man United (kushoto) na alivyo sasa pichani kulia.
Ronaldo alivyokuwa 2008 na sasa 2013
Katika miaka mitano iliyopita, tumeshuhudia kubadilika kwa Cristiano Ronaldo kutoka mchezaji mwembamba alipokuwa na umri mdogo hadi kuwa mwenye misuli na nguvu nyingi. 

Ronaldo alikuwa na uzito wa kg 78 msimu wa mwaka 2007/2008 klabuni Manchester United, na ameongezeka kilo 6 zinazomfanya sasa awe na kilo 84 huku urefu wake ukibaki kuwa futi 6 na inchi 1 (sawa na mita 1.86). 

Kuna mabadiko makubwa, kama ambavyo tumeshuhudia kutoka kwa Cristiano Ronaldo ambaye alihitaji ujanja mwingi wa chenga, 'kupiga vibaiskeli' na kumiliki mpira ili kumpita mtu, hadi kuwa Ronaldo mpigamabao ambaye anacheza soka la moja kwa moja na lenye kutumia nguvu.
Messi in 2008 and 2013
Lionel Messi wa Barcelona alivyokuwa mwaka 2008 (pichani kushoto) na alivyo sasa 2013 pichani kulia.
Messi alivyokuwa 2008 na sasa 2013
Messi kwa upande mwingine, amefanya mabadiliko kidogo, akiongeza kilo 2 tu za uzito wake (lakini mabadiliko makubwa akiyafanya kwenye mwili wake wa juu kwa kujiimarisha kuanzia kiunoni kwenda juu kwa kuinua vyuma na kujenga misuli) tangu aliposhiriki katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2008. 

Alikuwa na uzito wa kilo 65 mwaka 2008, na sasa ana kilo 67 huku urefu wake ukiwa haujabadilika, akiwa na futi 5 na inchi 7 (sawa na mita 1.7). 

Staili yake ya kucheza imebaki vile vile aking'ara kutokana na uwezo wake wa kushambulia, ingawa amepungua kasi ile aliyokuwanayo alipofunga goli kama la Maradona (CLICK HAPA UONE VIDEO YA GOLI HILO LA HATARI ALILOFUNGA) mwaka 2007 wakati akiwa na umri wa miaka 19.

Hivyo maswali ni kwamba ni kilogramu ngapi hasa ambazo Neymar anapaswa kuongeza ili atimize malengo yake? 

Runco kwa maoni yake, Neymar anapaswa kuwa na kg. 68. Jambo hilo litakuwa muhimu sana kwake katika kumudu soka la Ulaya, na Tito Vilanova, pamoja na menejimenti, watanufaika sana kama atafuata njia sahihi.

No comments:

Post a Comment