Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah |
Naomba nitoe ufafanuzi ufuatao baada ya kuona press ilivyokuwa:
Sababu kwa nini Tenga asizuie mashindano
--Tenga ni rais wa CECAFA na walioamua kuwa mashindano yafanyike Darfur ni mkutano mkuu uliopata taarifa ya hali ya usalama kwenye mkutano mkuu wa dharura uliofanyika Mauritius Mei 29, 2013 hivyo hawezi kukiuka maamuzi ya General Assembly. Tanzania inayo haki ya kuzuia timu zake zisishiriki lakini haina haki ya kuzuia mashindano yasifanyike kwa kuwa nchi nyingine zinaweza zikaona hali ya usalama ni nzuri.
--Kuhusu El Mereikh kujitoa
Hadi wakati wa Press Conference, Tenga kama rais wa CECAFA alikuwa hajapata hizo taarifa na aliwahakikishia waandishi kuwa kila baada ya masaa mawili anapokea taarifa kuhusu maendeleo ya maandalizi. Alisisitiza mwandishi aliye na uhakika wa habari hizo za kujitoa kwa klabu hizo, aandike ili aisaidie serikali kufanya maamuzi
--Kikao na serikali
Tenga alieleza kuwa juzi TFF ilikutana na serikali, kwa maana ya Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Michezo, na wadau wengine wa usalama na TFF ikatoa taarifa za maendeleo ya maandalizi, ikiwa ni pamoja na kueleza klabu za Simba na Yanga zitafikia wapi, usalama utakuwa wa aina gani, zitachezea viwanja gani, usafiri wa ndani utakuwaje na uhakika wa usalama kutoka serikali ya Sudan. Serikali baada ya kupata taarifa hizo imesema itathmini na kutoa tamko
--Ukaguzi
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye, alifanya ziara ya wiki moja kwenye majimbo hayo na kukagua viwanja na hoteli. Tenga alisema viwanja vipo na hoteli zipo na taarifa hizo zimewasilishwa serikalini. Alisema walioangalia televisheni waliona wakati Musonye akifanya ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment