Thursday, May 2, 2013

BAYERN YAIDHALILISHA BARCA KUIFUATA DORTMUND FAINALI UEFA

Robben akishangilia na wenzake
Gerard Pique (kushoto) akijiuliza na kipa Valdes baada ya kufungwa
Baba Shakira akiwa hoi baada ya kujifunga goli la pili
Thomas Muller akifunga la tatu
Shabiki aliyevamia uwanjani akienda kumkumbatia Ribery

Shabiki aliyevamia uwanjani akimkumbatia Ribery
Shabiki aliyevamia uwanjani na kumkumbatia Ribery akitolewa na polisi. Ribery anamkabidhi jezi yake
Muuaji Robben akishangilia

BARCELONA, Hispania
BAYERN Munich wametinga katika fainali ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itakayokutanisha Wajerumani watupu wakati walipoisambaratisha Barcelona 3-0 kwenye Uwanja wa Nou Camp na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 7-0.


Mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu ya Ujerumani waliimaliza mechi mapema wiki iliyopita kwa ushindi wa 4-0 nchini Ujerumani na hapakuwa na namna ya kufufuka kwa Wahispania hao wakati Arjen Robben alipofunga goli la kuongoza dhidi ya kipa Victor Valdes katika dakika ya 49.


Kudhalilika kwa Barca kulikamilishwa mwishoni mwa mechi wakati Gerard Pique alipojifunga mwenyewe na Thomas Mueller, ambaye alifunga magoli mawili katika mechi yao ya kwanza, akapachika la tatu kwa kichwa.


Barca, kama Bayern ambao wanafukuzia taji la tano la Ulaya, wanategemea kipaji cha Lionel Messi, ambaye anarejea kutoka katika majeraha ya misuli ya nyuma ya paja na ambaye aliachwa benchi, lakini bila ya Mwanasoka Bora wa Dunia huyo hawakuwa na makali yoyote.


Bayern watacheza dhidi ya Borussia Dortmund katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Wembley mjini London Mei 25 baada ya Dortmund kuitoa Real Madrid kwa jumla ya mabao 4-3 Jumanne.

No comments:

Post a Comment