Saturday, April 13, 2013

YANGA, OLJORO 'LIVE' SUPERSPORT LEO

Kutoka kushoto Nadir Harob 'Cannavaro', Didier Kavumnbagu, Simon Msuva na Mbuyu Twite wakishangilia katika moja ya mechi za timu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom baina ya Yanga na JKT Oljoro itarushwa moja kwa moja leo kupitia kituo cha televisheni cha Supersport.

Mpambano huo ni kati ya mechi mbili za Ligi Kuu ya Bara zitakazopigwa leo, nyingine itakuwa ni baina ya Prisons na Ruvu Shooting.

Wakati mechi ya Yanga dhidi ya Oljoro itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, pambano baina ya Prisons na Shooting litafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Vinara wa ligi Yanga wenye pointi 49, watakuwa wakijaribu kurejesha pengo la pointi kileleni dhini ya wanaosdhika nafasi ya pili Azm kuwa pointi 6, baada ya wapinzani wao hao wa mbio za ubingwa kushinda 3-1 dhidi ya African Lyon katikati ya wiki na kufikisha pointi 46.

Mabingwa Simba ambao wameshapoteza matumaini ya kutetea taji wakiwa wanashika nafasi ya nne watakuwa na mtihani mkubwa kesho Jumapili dhidi ya Azam katika mechi ambayo Yanga watakuwa upande wa mahasimu wao katika moja ya matukio adimu sana katika historia yao ya upinzani wa jadi nchini wakiwaombea wawafunge "Wanalambalamba" ili wazidi kulikaribia kombe.

 

No comments:

Post a Comment