Tuesday, April 30, 2013

MECHI YA SIMBA, POLISI MOROGORO YAINGIZA MIL 18/-

Haruna Chanongo (kushoto) wa Simba akiwania mpira dhidi ya Abdallah Mfuko wa Polisi Morogoro wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.

Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.

Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.

No comments:

Post a Comment