Monday, March 4, 2013

TAZAMA WAKENYA WANAVYOENDELEA KUPIGA KURA LEO KUMPATA MRITHI WA MWAI KIBAKI ANAYEACHIA NGAZI... MAMILIONI WAJITOKEZA... MCHUANO NI MKALI KATI YA MAWAZIRI WAKUU WA SASA UHURU KENYATTA NA ODINGA

Nachukua... nawekaa... waaaa! Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea urais, Uhuru Kenyatta akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura cha eneo la Gatundu nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya wanaendelea kupiga kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi nafasi inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa, ushindani mkali upo baina ya Uhuru na Raila Odinga. (Picha: Reuters)
Safari hii piga ua lazima nishinde...! Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea urais kupitia Coalition for Reforms and Democracy (CORD), Raila Odinga akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura cha Kibera, Nairobi nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya wanaendelea kupiga kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi nafasi inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa, ushindani mkali unaonekana kuwapo kati ya Odinga na Uhuru Kenyatta. (Picha: Reuters)
Odinga akijaindaa kupiga kura yake

Uhuru akiendelea na mchakato wa kumchagua mbunge wa Gatundu

Wananchi wa Kenya wakipanga foleni kupiga kura katika jiji la Nairobi, leo Machi 4, 2013.

Shoto-kulia-shoto- kulia...! Askari akisimamia foleni wakati wananchi wa Isiolo nchini Kenya wakiendelea kupiga kura kumchagua rais mpya wa Kenya leo leo Machi 4, 2013.

Hapa ni ahdi kieleweke...! Wananchi wa Kenya wakiwa katika foleni ndefu kuhakikisha kuwa wanapiga kura kumchagua rais wao leo Machi 4, 2013

Waangalizi mbalimbali wa kimataifa wakifuatilia uchaguzi wa Kenya leo Machi 4, 2013. Hapa ni aktika kituo kimojawapo cha eneo la Isiolo.

Mwananchi wa Kenya akipiga kura yake kwa siri kumchagua rais mpya wa nchi yao leo Machi 4, 2013


 Na mimi jamani.... bibi naye akipiga kura leo kumchagua rais mpya wa Kenya atakayemrithi Mwai Kibaki.Nipisheni... zamu yangu jamani! Wananchi wa Kenya wakiendelea kujipanga kabla ya kupiga kura kumchagua rais wao mpya leo Machi 4, 2013.

Kama mpira wa kona vile....! Mgombea wa urais wa Kenya, Raila Odinga akiwa amezungukwa na waandishi wa habari mara tu baada ya kupiga kura yake leo Machi 4, 2013. Kwa utulivu na utii....wananchi wakipanga foleni kwa nia ya kupiga kura kumchagua rais mpya wa Kenya leo Machi 4, 2013. 
No comments:

Post a Comment