Tuesday, March 19, 2013

SAMATA, ULIMWENGU WARIPOTI STARS

Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Taifa Stars, Mbwana Samatta akimtoka beki wa Ivory Coast, Alexandre Lolo wakati wa mechi yao ya hatua ya awali kufuzu kwa Kombe la Dunia kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, mjini Abidjan. Stars ililala 2-0.

Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.

Ujio wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti kambini leo asubuhi.

Wachezaji John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri. Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia nayo wenzao kuwa imejaa.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Kim Poulsen leo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Mazoezi hayo yataanza saa 9 alasiri.

No comments:

Post a Comment