Sunday, March 3, 2013

REAL MADRID ILIYOJAZA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA PILI KAMA MORATA, ESSIEN NA CALLEJON ILIVYOITESA TENA BARCELONA ILIYOCHEZESHA WAKALI WAKE WOTE KAMA LIONEL MESSI, INIESTA, PEDRO, BUSQUETS, PIQUE, DANI ALVES, VALDES, DAVID VILLA NA JORDI ALBA... BAADA YA USHINDI, MOURINHO ASHANGAZA WENGI KWA KUAMUA KUPELEKA KIKOSI CHAKE KWENYE UWANJA WA MAN CITY (ETIHAD) KUJIANDAA DHIDI YA MAN U JUMANNE...!

Mess akijaribu kukipita kitoto Morata cha Madrid kilichotoa krosi ya goli lililofungwa na Karim Benzema.
Essien naye alishiriki kuiangamiza Barca
Ramos akimzidi Pique na kufunga goli la ushindi la Real
Benzema akishangilia goli la kwanza aliloifungia Real dhidi ya Barca.
Benzema akipongezwa na Callejon na Kaka

Messi akishangilia goli la kusawazisha
Tunatishaaaaaa....! Ramos akishangilia baada ya kufunga goli la ushindi
Barca siku hizi kwetu mdebwedooooo...! Ramos akishangilia na Luka Modric
Kwanjaaa...! Albeloa akimkwatua Pedro wa Barca
Ishakuwa soo....! Messi akiskitika baada ya Ramos kuwadungua Barca goli la pili
Huna 'nizamu' .... kipa Victor Valdes wa Barca akilimwa kadi nyekundu kwa kumkoromea refa baada ya mechi kumalizika akilalamikia kutopewa penati

Real Madrid, ambayo ushindi wake wa 3-1 kwenye Uwanja wa Camp Nou Jumanne iliyopita uliifikisha fainali ya Kombe la Mfalme kwa kuing'oa Barcelona kwa jumla ya mabao 4-2, imeendelea kuionea Barca kwa kuifunga kwa mara ya pili mfululizo nndani ya siku nne, safari hii kwa mabao 2-1 katika mechi yao ya raundi ya 26 ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Ushindi huo ulipunguza tofauti ya pointi baina ya Real inayokamata nafasi ya tatu kwenye msimamo na vinara Barcelona kuwa pointi 13.

Sergio Ramos ndiye aliyefunga goli la ushindi kwa kichwa akitumia vyema kona iliyopigwa kiufundi na Luka Modric katika dakika ya 82. Mfaransa Karim Benzema alianza kwa kufunga goli la utangulizi katika dakika ya sita na Muargentina Lionel Messi akaisawazishia Barca katika dakika ya 18.

Awali, ushindi huo wa Real haukutarajiwa kwani wachezaji wengi waliopangwa si wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichoshinda 3-1 dhidi ya Barca Jumanne iliyopita. Baadhi ya wachezaji wa akiba wa Real walioanza kikosini na kuibuka na ushindi huo ni yosso Morata, Michael Essien, Callejon, Luka Modric na Kaka huku Sergio Ramos akichezeshwa katika nafasi ya beki wa kulia na Pepe akiwa kiungo mkabaji.

Real iliwaacha nje ya kikosi kilichoanza nyota wake kadhaa kwa sababu ya kuhofia kuumia kabla ya mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Man U itakayopigwa keshokutwa Jumanne. Cristiano Ronaldo, Albeloa na Sami Khedira walianzia benchi huku nyota wengine wa kikosi cha kwanza kama Mesut Ozil na Gonzalo Higuain wakikosekana kabisa, kama ilivyo kwa Angel di Maria aliyekuwa akitumiki adhabu.

Tofauti na Real, Barcelona walipanga kikosi chao kamili, wakikosekana Xavi anayesumbuliwa na jeraha la paja, Cesc Fabregas aliyeonekana kucheza kwa kiwango cha chini katika el clasico iliyopita ambayo walichapwa nyumbani kwao mabao 3-1 pamoja na Cares Puyol.

Lionel Messi, Andres Iniesta, Sergio Busquets, Dani Alves, Jordi Alba, David Villa, Pedro, Gerrard Pique na Victor Valdes ni miongoni mwa wakali wao walioanza kikosini.

Barca nusra wapigwe goli la tatu wakati 'fri-kiki' kali ya Ronaldo ilipogonga mwamba na kurudi uwanjani katika kipindi cha pili huku kipa Valdes akiokoa bao la wazi wakati alipobaki na 'dogo' Morata ambaye alipiga shuti kichovu na mpira kupanguliwa naye (Valdes) na kuwa kona.

Barca walililia kupewa penati katika dakika za majeruhi baada ya Adfriano kuonekana kuwa aliangushwa na Ramos; malalamiko ambayo mwishowe yalimfanya Iniesta alimwe kadi ya njano na kipa Valdes alimwe kadi nyekundu licha ya mechi kuwa tayari imeshamalizika.

Kama kawaida, ni Barca ndiyo waliomiliki zaidi mpira (asilimia 76), lakini ni wao pia ndiyo walioonekana kushambuliwa zaidi na mwishowe kufungwa kama ilivyokuwa katika clasico iliyopita waliyopigwa 3-1 na pia dhidi ya AC Milan katika klabu Bingwa Ulaya iliyochezwa Februari 20 na kuchapwa mabao 2-0 licha ua kumiliki mpira kwa asilimia 65, kucheza pasi zaidi ya 650 na kuishia kupiga mashuti mawili tu ya kulenga goli katika dakika zote 90 kulinganisha na mashuti sita ya Milan iliyocheza pasi sahihi 261 tu.
 
KUJIFUA MAN CITY
Real Madrid wamechukua hatua ya kushangaza baada ya kuthibitisha kuwa watakwenda kujifua kwenye Uwanja wa Etihad wa klabu ya Manchester City kujiandaa na mechi yao ya marudiano ya hatua ya 16-bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya watakayocheza keshokutwa (Jumanne Machi 5, 2013) dhidi ya Manchester United.

Kwa kawaida, kila klabu hulazimika kueleza mbele ya mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi yao kabla ya mechi.

Jana, ilithibitishwa kuwa Real ingebaki Hispania kwa maandalizi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Man U.

Hata hivyo, mipango hiyo sasa imebadilishwa na kocha Jose Mourinho wa Real ameamua kuwa kikosi chake kijifue kwenye uwanja wa mahasimu wa Man U, klabu ya Man City ambayo inashikilia ubingwa wa ligi kuu ya England.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na sababu za Real kuchagua kwenda kujifua kwenye uwanja wa Man City.

No comments:

Post a Comment