Neymar |
Neymar |
Neymar |
Neymar |
Neymar |
Neymar |
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akilinganishwa na Pele, lakini gwiji huyo mwenye umri wa miaka 72, ambaye daima alikuwa akidai kwamba Neymar ni bora kuliko mwanasoka bora wa dunia mara nne mfululizo, Lionel Messi, amemgeuka akidai yosso huyo anapewa sifa kubwa mno kuliko anazostahili.
"Kwa timu ya taifa, yeye ni mchezaji wa kawaida sana," Pele aliliambia gazeti la O Estado de Sao Paulo.
"Ana majukumu makubwa lakini anachojali ni kubadili ni staili yake na mitindo ya nywele.
"Kila mechi tunayoenda kucheza nje ya nchi, hachezi vizuri. Kila mtu anadhani kwamba yeye ndiye anayepaswa kuwa jibu la matatizo yetu yote yaliyopo kwenye timu yetu ya taifa [lakini] Neymar hayuko tayari kubebeshwa mzigo mkubwa kiasi hicho, hawezi kuubeba."
Pele kisha akaongeza kwamba anaamini kuwa kiwango cha kufadhaisha cha Neymar kwenye timu ya taifa ya Brazil, ambacho ni tofauti na anachoonyesha kila siku akiwa na klabu yake ya Santos, ambako ameshatwaa Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Amerika Kusini la "Copa Libertadores", linatokana na kukosa uzoefu wa mbinu za Ulaya.
"Hajawahi kucheza soka nje ya nchi, na soka la Ulaya ni tofauti na tunalocheza hapa Amerika Kusini," aliendelea.
"Anapenda kukaa na mpira, kupiga chenga, kuonyesha mbwembwe zake [lakini] anapaswa kuuacha mpira kidogo, acheze kwa ajili ya timu.
"Hana uzoefu kabisa wa kimataifa. Barcelona itakuwa ni timu nzuri kwake [lakini] sijui kama ataondoka kwa sababu Santos bado wanamuhitaji."
No comments:
Post a Comment