Sunday, February 3, 2013

PAMBANO LA YANGA, MTIBWA SUGAR LAINGIZA MIL 125/-


MECHI namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 imeingiza sh. 125,181,000.

Watazamaji 22,030 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,356,002.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 19,095,406.78.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 19,583 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 97,915,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,435,255.48, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 9,261,153.29, Kamati ya Ligi sh. 9,261,153.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,630,576.64 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,601,559.61.

No comments:

Post a Comment