Thursday, February 14, 2013

HISPANIA WADAI MAN UTD ILIBEBWA SARE 1-1 v REAL MADRID

Di Maria (kushoto) akianguka ndani ya boksi

RADIO ya Hispania imedai kuwa Manchester United ilibebwa katika sare ya 1-1 dhidi ya Real Madrid katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Radio hiyo ilidai kwamba matukio mawili ya utata ndiyo yaliyowapa sare, Man Utd katika mechi hiyo ambayo kipa wa Mashetani Wekundu, David de Gea, alisifiwa kwa kucheza kwa kiwango cha juu cha 'Man of the Match' kutokana na kuokoa mashuti nane ya hatari.

Matukio hayo mawili yametajwa kuwa ni Man Utd kupewa kona ambayo hawakustahili iliyozaa goli na pia Real Madrid kunyimwa penalti.

Refa Mjerumani, Brych ameelezwa kwamba alipaswa kuwapa Real Madrid penalti baada ya Phil Jones kumsukuma Angel Di MarĂ­a ndani ya boksi na kuwazawadia kimakosa Man Utd kona iliyozaa goli lao la kuongoza lililofungwa na Danny Welbeck baada ya Shinji Kagawa kuwa mtu wa mwisho kuugusa mpira hivyo ilipaswa kuwa 'goal kick'.

Katika mechi hiyo iliyosubiriwa kwa hamu, Real Madrid walisawazisha kupitia kwa nyota wa zamani wa Man Utd, Cristaino Ronaldo, ambaye alifunga kwa kichwa kama alivyo Welbeck goli la kuongoza.

No comments:

Post a Comment