Friday, February 15, 2013

GOLDIE WA PREZZO AFARIKI DUNIA

Goldie wa Nigeria (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafikiye rapa wa Kenya, Prezzo ndani ya jumba la Upville la Big Brother StarGame 2012.
Goldie wa Nigeria (kulia) enzi za uhai wake akiwa na Prezzo ndani ya jumba la Upville la Big Brother StarGame 2012.
Goldie alikuwa mcheshi sana

Mambo yake yalikuwa safi. Akisafiri kwa ndege alipanda "First Class". Hapa alikuwa akienda nchini Afrika Kusini katika moja ya shughuli zake

Goldie akiwa katika ndege

Ndani ya BBA House

Enzi zake kwenye Jumba la BBA
Goldie alipenda kufurahi kwa sababu maisha haya ni mafupi sana

Alipendelea kupika ndani ya BBA House

RAFIKI wa kike wa rapa Mkenya, Prezzo, aliyekutana naye kwenye jumba la Big Brother, muimbaji wa Nigeria aliyekuwa anainukia, Goldie Harvey, amefariki dunia.

Sababu za kifo chake bado hazijapatikana lakini vyombo vya habari vya Nigeria vimesema kuwa alifariki usiku wa kuamkia leo alipofikishwa katika hospitali ya Reddington iliyopo Victoria Island mjini Lagos mikononi mwa mikono ya rafikiye wa karibu Denrele baada ya kulalamikia maumivu ya kichwa huku taarifa nyingine zikidai kwamba alipatwa na pneumonia.

Goldie alikuwa ndiyo kwanza amerejea Nigeria kutokea Marekani ambako alienda kuhudhuria tuzo za Grammy Awards pamoja na bosi wa lebo yake ya kurekodi muziki ya Kennis Music, Kenny Ogungbe. Kenny St. Best, msanii mwingine ambaye yuko chini ya Kennis Music alithibitisha taarifa hizo.

Alisema: “Ni kweli. Bado nashinda kuamini. Bado niko katika mstuko."

Kifo chake ni cha ghafla. Mbali na fani yake iliyoanza kuchipua, Goldie alikuwa ni mtu mwenye upendo sana. Ni mzungumzaji mzuri na ujumbe wa meseji zake na 'email' zake daima ulikuwa ni wa kiupole.

Denrele na Goldie walikuwa marafiki wa karibu sana. Walikuwa wakitarajia kuzindua kipindi chao cha maisha halisi cha katika televisheni kiitwacho ‘Tru Friendship’ katika wiki chache zijazo.

Katika jumba la Big Brother, alimuangukia kimapenzi rapa Mkenya Prezzo kiasi cha kufikia kutapika wakati mmoja wakati rapa huyo alipomwambia kwamba wao ni marafiki tu. Prezzo baadaye naye alizama kwenye penzi la kimwana huyo na uvumi wa hivi karibuni ulidai kwamba wawili hao walikuwa wakijiandaa kufunga ndoa, taarifa ambazo zilikanushwa na Prezzo
.

1 comment:

  1. Huyu dada jamani mbona alikuwa kaolewa na mzungu na picha tumeziona.Iweje awe mchumba wa Prezo?!

    ReplyDelete