Friday, February 1, 2013

BECKHAM KUCHEZA BURE PSG, MALIPO YAKE YOTE KUCHANGIA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

David Beckham akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza amesaini mkataba wa miezi mitano na klabu ya Paris Saint-Germain.

DAVID Beckham amejiunga na klabu ya PSG ya Ligi Kuu ya Ufaransa na ametangaza kwamba atacheza huko bure.

Kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England mwenye umri wa miaka 37, amesaini mkataba wa miezi mitano na atachangia mshahara wake -- ambao ni angalau paundi milioni 1 (Sh. bilioni 2.5) - kwa mfuko wa jamii.

"Nina furaha sana, ni jambo ambalo nilikuwa nikilifanyia kazi na kulinguzumzia kwa muda mrefu," alisema jana.

"Sitachukua mshahara wowote. Mshahara wangu wote utakwenda kwenye kituo cha kulelea watoto. Hilo ni moja ya mambo tunayofurahia na tunajivunia kuyafanya."

Aliongeza: "Ni jambo ambalo jamaa [menejimenti ya PSG] wanafanya, lakini hela ndefu. Hayo ni kati ya mambo yanatufurahisha sana. Kuweza kutoa kiasi kikubwa kwa mfuko wa kulelea watoto mjini Paris ni jambo kubwa."

Beckham amekuwa hana klabu tangu alipoondoka katika klabu ya Los Angeles Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu Duniani Desemba na amekuwa akijifua na timu ya Arsenal.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England alikuwa na ofa kutoka katika klabu 12 tofauti lakini amechagua kujiunga na klabu hiyo inayomwaga pesa ya PSG.

Licha ya kusema hivi karibuni kwamba anaweka makazi yake ya kudumu mjini London, Beckham daima alisisitiza kwamba atatoa maamuzi yake ya klabu atakayohamia kwa kuzingatia "sababu za kimichezo".

PSG imemwaga zaidi ya paundi milioni 200 katika miezi 18 iliyopita, na inafundishwa na kocha Carlo Ancelotti - ambaye alikuwa akiifundisha AC Milan wakati Beckham alipotua katika klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. Bado wamo kwenye michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na wataikabili Valencia ya Hispania katika hatua ya 16-Bora.

No comments:

Post a Comment