Friday, January 11, 2013

STERLING AZUNGUMZIA UVUMI KWAMBA ANA "WATOTO WATANO"

Raheem Sterling
Mellissa Clarke akiwa na mtoto wa Sterling, Melody Rose
Picha ya Melody Rose iliyotumwa na Mellissa

YOSSO wa Liverpool, Raheem Sterling (17) amefafanua kuhusu ripoti zilizozagaa kwamba amezaa watoto WATANO na wanawake tofauti na kwamba mtoto wa sita yuko tumboni anakuja!

Anaye mtoto mmoja wa kike, Melody Rose, aliyezaliwa miezi saba iliyopita baada ya kuwa na mahusiano mafupi na mwanamke aitwaye Mellissa Clarke (23). Mtoto huyo alizaliwa wakati Sterling akiwa na umri wa miaka 16.

Sterling aliliambia gazeti la Mirror: "Baadhi ya mambo yanaandikwa unashangaa. Unasoma mambo kama vile nina watoto watano na kwamba mwingine yuko njiani. Ni upuuzi na uongo kabisa.

“Niliona ni kama ucheshi hata kulifikiria tu suala hilo. Uvumi ukianza unakua hadi unafikia pabaya.

"Huwa nacheka tu kuhusu baadhi ya mambo wanayosema watu.

"Lakini sina cha kujutia. Ni jambo gumu kwangu. Nataka kuweka akili yangu kwenye soka kwa sababu mimi bado ni mdogo sana. Hakika ni ngumu kwangu kuwa mweledi zaidi kama nitaendelea kuishi hivi ninavyokwenda sasa. Hilo ni muhimu sana kwangu."

Mellissa amekuwa akituma picha kwenye internet akimshukuru Sterling kwa kumfanya kuwa mama. "Asante kwa kunifanya kuwa mama wa binti huyu mrembo mdogo @Sterling31" aliandika Mellissa katika ukurasa wake wa Twitter.

Sterling aliwasili Uingereza akitokea Jamaica akiwa na umri wa miaka mitano. Alikulia katika mazingira ya kimasikini katika eneo la Wembley, Kaskazini Magharibi mwa London, kisha akajiunga na QPR.

Liverpool ilimsajili akiwa na umri wa miaka 15 tu mwaka 2010 kwa ada ya uhamisho ya paundi 600,000 ambayo itaongezeka hadi kufikia paundi milioni 5 kulingana na idadi ya mechi atakazocheza.

Alihamia mjini Merseyside akiwa na mama yake na nduguze watatu. Msemaji wa klabu alisema: "Hili si jambo tunalohitaji kulizungumzia." 

No comments:

Post a Comment