Friday, January 18, 2013

ROONEY ASIPEWE TENA PENALTI, ASEMA ROY KEANE

Wayne Rooney wa Manchester United akipaisha penalti wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya West Ham United kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England juzi Januari 16, 2013.

GWIJI wa Manchester United, Roy Keane anaamini kwamba Wayne Rooney HATAPIGA TENA penalti ya klabu hiyo!

Rooney alikosa penalti wakati wa mechi yao waliyoshinda 1-0 dhidi ya West Ham United katika Kombe la FA Jumatano.

Nahodha wa zamani wa Man United, Keane alisema: "Kocha atakasirika sana. Ile itakuwa ni penalti ya mwisho kwa Rooney kuipiga kwa United."

No comments:

Post a Comment