WAYNE Rooney alifunga goli moja na kukosa penalti katika siku ambayo alirejea kutokea kwenye majeraha wakati Manchester United ilipotinga raundi ya nne ya Kombe la FA baada ya kuibwaga West Ham 1-0.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya England, alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza tangu Krismasi, alifunga kutokea jirani na lango na kuwafanya wenyeji waongoze.
West Ham walinyimwa penalti wakati mpira uliopoonekana kupiga mkono wa Rafael ndani ya eneo la penalti.
Lakini katika usiku wa matukio mchanganyiko, Rooney alipaisha penalti juu ya lango na kusababisha mechi hiyo kwenye Uwanja wa Old Trafford imalizike roho zikiwa juu katika dakika za lala salama.
Matt Taylor alikaribia kufunga kwa upande wa West Ham, lakini wenyeji walisimama kidete na kushinda mechi hiyo na sasa watawakabili Fulham Januari 26 au 27.
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alisema kuhusu rekodi ya timu yake ya kufunga penalti tano na kukosa nne msimu huu: "Nadhani tunahitaji kuboresha katika eneo hilo.
"Kuna mifano mingi mizuri ya magwiji kwa miaka kadhaa -(kiungo wa zamani wa Southampton) Matthew Le Tissier alifunga penalti 47 kati 48 alizopiga katika maisha yake ya soka la kulipwa.
"Penalti ni fursa yako kuwaadhibu wapinzani kwa faulo, kushika mpira ndani ya boksi ama vyovyote kwa kufunga goli."
Vikosi:
Manchester United
- 13 Lindegaard
- 02 Rafael
- 04 Jones
- 12 Smalling
- 28 Buttner
- 07 Valencia
- 08 Anderson (Carrick - 67' )
- 11 Giggs
- 17 Nani (Scholes - 77' Booked )
- 10 Rooney
- 14 Hernandez
Wa akiba
- 40 Amos
- 05 Ferdinand
- 16 Carrick
- 22 Scholes
- 26 Kagawa
- 19 Welbeck
- 20 Van Persie
West Ham United
- 22 Jaaskelainen
- 02 Reid
- 05 Tomkins
- 27 Spence Booked
- 33 Potts
- 14 Taylor
- 21 Diame (Collison - 65' )
- 23 Diarra
- 32 O'Neil
- 09 Cole (Nolan - 65' Booked )
- 12 Vaz Te (Lee - 78' )
Wa akiba
- 30 Spiegel
- 20 Demel
- 04 Nolan
- 07 Jarvis
- 10 Collison
- 43 Lletget
- 47 Lee
Refa: Dowd
Mashabiki: 71,081
No comments:
Post a Comment