Saturday, January 19, 2013

REMY: QPR IKISHUKA DARAJA NATIMKA ZANGU


Straika mpya QPR, Loic Remy akipozi na jezi ya klabu yake mpya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza kusajiliwa kwake klabuni hapo jana Januari 18, 2013 mjini Harlington, England.

Straika mpya QPR, Loic Remy akipozi na kocha Harry Redknapp na jezi ya klabu yake mpya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza kusajiliwa kwake klabuni hapo jana Januari 18, 2013 mjini Harlington, England.

Straika mpya QPR, Loic Remy akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza kusajiliwa kwake klabuni hapo jana Januari 18, 2013 mjini Harlington, England.
Loic Remy wa Queens Park Rangers akishiriki mazoezi jana Januari 18, 2013 mjini Harlington, England.

Loic Remy wa Queens Park Rangers akishiriki mazoezi jana Januari 18, 2013 mjini Harlington, England.

STRAIKA Loic Remy aliyesajiliwa QPR kwa dau lililoweka rekodi mpya kwa klabu hiyo, amesema huenda akatimka zake iwapo watashuka daraja.

Alipobanwa ili aeleze kama atabaki QPR kama watashuka daraja msimu huu, Remy alisema akili yake ameiweka kwenye kukisaidia kikosi cha kocha Harry Redknapp kisishuke daraja.

Alisema: "Niko hapa kwa sasa na sitaki kufikiria kushuka daraja kwa sababu sitaki kuifikiria hali hiyo.

"Haya ni mambo ambayo yako nje ya uwanja. Kama suala hilo litafika, wakala wangu na QPR watakaa chini na kulizungumzia.

"Lakini sitaki kuzungumzia kuhusu kushuka daraja ama vipengele vya mkataba wangu, ninachotaka ni kuinuka na kukimbia.

"Huu ni wakati wa kuonyesha nini naweza kukifanya, kuwaonyesha walioniamini nini naweza kukifanya, kwamba Loic Remy ni mchezaji mzuri."

No comments:

Post a Comment