Monday, January 14, 2013

GOLI LA MAN UTD LILILOWAUA LIVERPOOL LILIKUWA LA "OFFSIDE"

USHAHIDI: Picha za video zinaonyesha kwamba Vidic alikuwa ameotea wakati alipougusa mpira wa mwisho wa goli
Vidic akiubadili mwelekeo mpira wa kichwa wa Evra na kuutumbukiza wavuni mwa Liverpool

REFA wa zamani wa Ligi Kuu ya England, Graham Poll amesema teknolojia inapaswa kuwekwa haraka baada ya picha za marudio za video kuonyesha kwamba beki Nemanja Vidic (31) alikuwa ameotea wakati alipokuwa mtu wa mwisho kuugusa mpira ulioingia wavuni kwa goli la pili na kuipa Manchester United ushindi wa 2-1 dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Old Trafford jana.

Howard Webb na timu yake ya waamuzi itakuwa imekwenda kwenye chumba chao cha kuvalia na kujadili mechi hiyo na zaidi mambo makubwa yaliyoamua mechi hiyo.

Wataridhishwa na kazi yao kwa ujumla wake isipokuwa maamuzi kadhaa waliyobofoa ya kona na 'fri-kiki'.

Lakini kubwa watabaini kwamba wanahitaji msaada wa teknolojia ili kupunguza kuiumiza timu moja na kuinufaisha nyingine kwa makosa ambayo ni ya kibinadamu kama goli la pili la Manchester United.

Vidic aliubadili mwelekeo kidogo kwa kichwa mpira wa kichwa kutoka kwa Patrice Evra na kuwapa goli la ushindi ambalo video zinaonyesha Vidic aliyeugusa mpira wa mwisho alikuwa ameotea.

No comments:

Post a Comment