Saturday, January 12, 2013

FERGIE AMWAMBIA REFA WEBB AMUANGALIE SUAREZ KESHO

Luis Suarez
Howard Webb

Sir Alex Ferguson

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anataka refa Howard Webb amuangalia kwa jicho la karibu straika wa Liverpool, Luis Suarez katika mechi yao ya kesho.

Fergie amemtaka Webb na wasaidizi wake kumuangalia sana straika huyo wa Uruguay.

Kocha Fergie alisema: “Kijana anaambatana na matukio ya utata. Sijui kama anayafurahia au hapana ila ni jambo ambalo tunatumai kwamba halitatuangukia nasi na kutuathiri."

Lakini kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amedokeza matukio jinsi yalivyokwenda kinyume nao wakati walipocheza dhidi ya Man United mara ya mwisho na kumshuhudia Jonjo Shelvey akitolewa kwa kadi nyekundu ya kuonewa.

Man United walishinda kwa penalti ya utata kwenye Uwanja wa Anfield.

Rodgers alisema: "Tunatumai kwamba maamuzi hayatatuonea kama ilivyokuwa katika mechi ile.

"Kadi nyekundu na penalti vilitugharimu. Natumai hawatapata maamuzi ambayo yanachangia matokeo."

No comments:

Post a Comment