Wednesday, December 5, 2012

VODACOM KUPAMBA SWAHILI FASHION WEEK


KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ni miongoni mwa wadhamini watakaorembesha na hatimaye kufanikisha tamasha la tuzo za Swahili Fashion Week 2012 litakalofanyika kuanzia kesho hadi keshokutwa.


Waandaaji wa tuzo hizo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati tayari walishatangaza majina ya waliopendekezwa kushiriki katika kuwania tuzo mbalimbali za Swahili Fashion Week 2012 ikiwa pamoja na njia zinazotumika kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa alisema wapenzi wa mitindo nchini wanaweza kununua tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo kwa kupitia huduma yao ya M-Pesa.
Alisema tiketi hizo zinauzwa kwa Sh. 20,000 kwa ili mpenzi anaweza kununua kupitia namba +255 767 22 24 41.
 

Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zinazoenda pamoja na sherehe ya miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa, mwaka huu zimeongezwa tuzo nyingine tatu kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweka changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo nchini na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati.
Jumla ya tuzo 15 zitawaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.
 

Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year, East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality, Stylish Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion TV Program of the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion Photographer of the Year, Fashion Journalist of the Year, Best East African Journalist (Mpya) na Upcoming Designer.
 

Twissa alisema: "Mchakato mzima wa kuchagua mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012 unasimamiwa na PUSH Mobile ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa namba ya mshiriki (CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba 15678, huku mchakato mzima wa kuzihakiki kura hizo utafanywa na PKF. Lakini pia kura zinaweza kupigwa kupitia blogu maalum ya kupigia kura ya www.sfw2012awards.blogspot.com."

Washindi wote wa tuzo za Swahili Fashion Week 2012 watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili Fashion Week, Jumamosi ya Desemba 8, 2012 katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Tanzania.


Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na: Vodacom, EATV, East Africa Radio, USAID Compete, Origin Africa, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania),  Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.

No comments:

Post a Comment