Friday, December 28, 2012

RONALDO MECHI 5 ZA MWISHO NJANO 5


BUNDI aliyelia Real Madrid si tu kwamba ameathiri matokeo, bali pia tabia za wachezaji.

Kutokana na presha, wachezaji hawachezi vizuri na wanaishia katika fadhaa. jambo hili limeonekana kwa Cristiano Ronaldo, ambaye alipewa kadi za njano tano katika mechi tano mfululizo za mwisho (dhidi ya Ajax, Valladolid, Celta, Espanyol na Malaga) ambazo zimemfanya kukaribia kufungiwa mechi moja kwa adhabu ya kadi 5 kwenye ligi, ambako tayari ana kadi nne.

Jambo hili linatia shaka unapoangalia mabadiliko ya tabia ya Cristiano katika suala la nidhamu katika mechi chache za mwisho, kulalamika kwa mwamuzi, kuhusika katika malumbano na wachezaji, kama ilivyotokea dhidi ya Hugo Mallo wa Celta Vigo, ambayo ingeweza kumfanya atolewe kwa kadi nyekundu.

Dhidi ya Ajax, Celta na Espanyol alipewa njano kwa kucheza faulo, ugenini dhidi ya Valladolid kwa kujibizana na ugenini dhidi ya Malaga kwa kushika mpira. Mechi tano mfululizo, kadi za njano tano, ni nyingi mno kwa mchezaji mkubwa kama Cristiano Ronaldo, ambaye ameonekana kwa muda mrefu kwamba amerekebisha tabia yake tangu msimu wa wake wa kwanza Real Madrid, ambao alitolewa kwa nyekundu mara mbili mfululizo.

No comments:

Post a Comment