Thursday, December 27, 2012

KLABU YA URUSI ILIAMUANDALIA MESSI OFA YA KUFA MTU


KLABU ya Urusi ambayo haitajwi jina ilitoa ofa ya kutisha ya euro milioni 90 kwa Lionel Messi ili aihame Barcelona wiki chache zilizopita, imebainika.

Gazeti la Hispania la El Mundo Deportivo limesema kabla ya Messi hajamwaga wino katika mkataba mpya mapema mwezi huu, baba wa mchezaji huyo, Jorge, alifuatwa na klabu ya Urusi iliyokuwa tayari kumlipa euro milioni 30 kwa mwaka kwa mkataba wa miaka mitatu.

Klabu hiyo ilikuwa pia imejiandaa kulipa ada iliyowekwa na Barca kama kipingele cha kuuvunja mkataba wake na klabu hiyo ya Catalunya ili nyota huyo akakipige Urusi.

Jorge Messi alimfikishia ofa hiyo mwanaye, lakini mchezaji huyo alikataa bila ya kusita na wala jambo hilo halikutajwa wakati wa maafikiano ya mkataba mpya na Barca.

No comments:

Post a Comment