Friday, December 14, 2012

BENZEMA ANAVAA "MAKUFULI" YA BEI MBAYA - CASILLAS

Mambo vipi mzee wa makufuli? Cassilas (kushoto) akisalimiana na mshkaji wake Benzema kabla ya kuanza kwa mechi yao ya robo fainali za Euro 2012 nchini Poland na Ukraine.


IKER Casillas ametoa siri ya katika chumba cha kuvalia cha Real Madrid. Kauli za kipa huyo zilijadilia pia nguo za ndani za Karim Benzema.

"Nguo za ndani za Benzema ni kibishoo. Zinakufanya usimame na kushangaa, ni kali sana, hivyo unaweza kubaini kwamba haziwezi kupita bila ya kujadiliwa katika chumba cha kuvalia. Lakini huyo ndiye Karim; ni mtu mwerevu linapokuja suala la mitindo ya nguo za ndani".

Casillas, ambaye pia alibainisha kwamba kwenye chumba cha kuvalia wanamuita "tikiti maji", pia alianika vikundi mbalimbali vya marafiki ndani ya kikosi chao. "Cristiano, Fabio na Pepe wanakuwa pamoja kwa muda mwingi, wanaenda pamoja kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, hivyo ndiyo maana wako karibu. Naweza kwenda mapumzikoni na Cristiano… lakini itabidi iwe ni safari iliyolipiwa gaharama zote!"

"Higuain na Di Maria hujichanganya na vijana wa Kihispania. Özil na Khedira wanachukua muda mrefu kidogo kuzoea, ingawa Sergio [Ramos] anazungumza sana na Özil. Yeye ni mpole sana na hasemi mengi. Daima huwa namtania. Anashindwa kuzungumza katika mikusanyiko na kwenye mikutano na waandishi wa habari".

No comments:

Post a Comment