Tuesday, December 18, 2012

ARSENAL YAUA 5-2, YAPANDA HADI NAFASI YA TANO... CAZORLA ATUPIA HAT-TRICK

Santi Cazorla wa Arsenal (katikati) akishangilia baada ya kufunga goli lake la tatu na la nne kwa Arsenal pamoja na Jack Wilshere (kushoto) na Alex Oxlade Chamberlain wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Santi Cazorla wa Arsenal (kushoto) akipongezwa na Jack Wilshere (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Santi Cazorla wa Arsenal (katikati) akishangiliana wachezaji wenzake  baada ya kufunga wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Santi Cazorla wa Arsenal (kushoto) akishangilia na Theo Walcott baada ya kufunga wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Santi Cazorla wa Arsenal akifunga goli lake la tatu wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Cazorla akipongezwa

Theo Walcott (kulia) na Thomas Vermaelen wa Arsenal wakipongezana baada ya mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Theo Walcott akishangilia baada ya kufunga wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

Theo Walcott wa Arsenal akifunga kwa mguu wa kushoto goli la tano la timu yake wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Madejski mjini Reading, England jana Desemba 17, 2012. Arsenal walishinda 5-2.

ARSENAL imeanza kutibu majeraha ya kutolewa kwa aibu katika mashindano ya Capital One Cup dhidi ya timu ya daraja la tatu ya Bradford City kwa ushindi wa kuvutia wa 5-2 ugenini dhidi ya Reading usiku wa kuamkia leo.

Lukas Podolski aliwafungia Arsenal goli la kuongoza la mapema na The Gunners walikuwa wakiongoza 4-0 baada ya dakika 60 wakati ya Santi Cazorla alipoibuka Mhispania wa tatu tu kufunga hat-trick katika ligi kuu ya England baada ya Fernando Torres na Jordi Gomez.
 

Arsenal bado wana mapungufu makubwa katika ulinzi, yaliyofanya washindwe kutoa kipigo kikali na badala yake kuwaruhusu Reading kurudisha magoli mawili 4-0, lakini Walcott aliongoza vyema mashambulizi.

Reading, walifunikwa mwanzo-mwisho, lakini waliamsha matumaini yasiyotarajiwa ya kuzinduka kufuatia magoli ya Adam Le Fondre na Jimmy Kebe waliofunga magoli mawili ndani ya dakika tano.

Lakini Theo Walcott, aliyecheza vyema katika eneo la kati la ushambuliaji, alifunga goli zuri la tano na kuiinua timu hiyo ya kocha Arsene Wenger hadi katika nafasi ya tano ya msimamo.

Katika jaribio la kupona kutoka katika kipigo cha aibu dhidi ya Bradford, matokeo haya yatawapa Arsenal kujiamini na morali - na yatasapoti madai ya Wenger kwamba timu yake bado ina mengi ya kutoa msimu.

Ulikuwa ni ushindi, ambao hata hivyo, unahitaji kutambulika kwamba ni dhidi ya timu inayochechemea ambayo, ambayo iko hatarini kuangukia kwenye ukanda wa hatari, ikiwa pointi sita tu juu ya timu za kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment