Saturday, December 29, 2012

ARSENAL YACHENJIWA NA BEKI MAPOU YANGA-MBIWA WA MONTPELLIER WANAYEMFUKUZIA KWA UDI NA UVUMBA... ASEMA NDOTO YAKE NI KUICHEZEA MAN UNITED TU...!

Bonge la beki....! Mapou Yanga-Mbiwa wa Montpellier akiwa kazini.
PARIS, Ufaransa
Beki anayefukuziwa na Arsenal kwa udi na uvumba, Mapou Yanga-Mbiwa wa Montpellier ya Ufaransa amesema anataka kuichezea klabu iliyo katika ndoto zake ya Manchester United.

Yanga-Mbiwa amekuwa pia akifukuziwa kwa muda mrefu na Chelsea.

Lakini alipoulizwa kuhusiana na matumaini yake kwa mwaka ujao wa 2013, beki huyo amekiri kwa kusema: Ndoto yangu ni kuteleza kwa magoti kiatika kona ya Old Trafford nikiwa mwilini na jezi ya Manchester United.

"Naichezea MU, klabu ninayoipenda na ninafunga goli linalotupa ushindi kwa kichwa kutokana na mpira wa kona. Ndiyo, hiyo itakuwa poa."

No comments:

Post a Comment