Monday, November 19, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI KUUAGA MWILI WA MAREHEMU MAKWETA… SPIKA MAKINDA, MBOWE NAO WASHIRIKI KUAGA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jackson Makwetta nyumbani kwake Bunju jijini Dar es Salaam leo.

Makwetta alifariki dunia juzi Jumamosi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Enzi za uhai wake, Makweta alikuwa   mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini kuanzia mwaka 1975 hadi 2010 alipong’olewa na Deo Sanga.

Aliwahi pia kuwa waziri katika wizara mbalimbali ikiwamo ya elimu, ofisi ya waziri mkuu, kilimo na utumishi.

Wengine waliohudhuria shughuli za kuuaga mwili wa Makweta ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anna Makinda na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.

Akitoa nasaha zake, Mhe. Makinda aliwataka viongozi wengine kujifunza kwa marehemu (Makweta) ambaye licha ya kudumu katika nafasi mbalimbali za juu serikalini, kamwe hakujihusisha na kujilimbikizia mali kwa njia haramu.

No comments:

Post a Comment