Thursday, October 4, 2012

MOURINHO AKUNWA NA KIWANGO ALICHOONYESHA KAKA DHIDI YA AJAX... ASEMA ALIFANYA UAMUZI SAHIHI KUMUANZISHA HUKU MESUT OZIL AKISOTEA BENCHI NA KUINGIA BAADAYE...!

Tobias Sana wa Ajax akianguka wakati akijaribu kumzuia Kaka kwenye mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya jana Oktoba 3, 2012 mjini Amsterdam, Uholanzi.

Kaka (kushoto) na Benzema wa Real Madrid wakishirikiana kumuacha Toby Alderweireld  wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya jana Oktoba 3, 2012 mjini Amsterdam, Uholanzi.
MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amekiri kukunwa na kiwango cha juu kilichoonyeshwa na Kaka katika mechi yao ya jana ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya waliyoshinda ugenini 4-1 dhidi ya Ajax.

Kaka alianzishwa katika kikosi cha kwanza badala ya Mesut Ozil.

Mourinho amesema: "Kaká alianza na Özil akawa mtokea benchi, ni jambo la kawaida. Niliifikiria mechi hii, wapinzani na kazi kubwa aliyoifanya wiki nzima na kuona kwamba ni jambo zuri kwake aanze dhidi ya Ajax. Watu wa vyombo vya habari huamini kwamba kila wakati mchezaji mwenye jina kubwa anapokuwa benchi inamaanisha kwamba kuna tatizo kubwa, kazi yangu ni kufikiri na kuamua nani acheze ili tupate matokeo mazuri. Napaswa kuchagua wachezaji 11 tu na hivyo mara zote kuna wengine watalazimika kuwa nje."

Katika mechi hiyo, Kaka alicheza kwa dakika 73 kabla ya kupumzishwa na ndiye aliyetoa pasi ya bao kali lililofungwa kwa 'tik-taka' na Karim Benzema.

No comments:

Post a Comment