Tuesday, October 23, 2012

MECHI YA MTIBWA SUGAR, JKT RUVU YAPELEKWA MBELE


MECHI namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 mwaka huu Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, sasa itafanyika Novemba 7 mwaka huu.

Mabadiliko hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3 mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa kwa mechi za Super Week zilizooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport cha Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment