Monday, September 10, 2012

ZIDANE: BENZEMA NI MOTO WA KUOTEA MBALI


Karim Benzema
MADRID, Hispania
Zinedine Zidane amesema anaamini kwamba limebaki suala la muda tu kabla straika Karim Benzema wa Real Madrid hajaanza kuonyesha tena kiwango chake cha juu.

Straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akihaha kufunga goli lake kwanza katika wiki za mwanzoni mwa msimu wa 2012-13, lakini Mfransa mwenzake Zidane bado anaamini kwamba mchezaji huyo ataanza tena kuwa mhimili wa mafanikio ya klabu yake na pia timu katika kikosi cha timu yake ya taifa.

"Benzema bado hajacheza katika tena kiwango chake cha juu, lakini dunia nzima inajua kwamba yeye ni mchezaji nyota," Zidane amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

"Ninachojua tu ni kwamba haitachukua muda mrefu kabla mwishowe hajarudi kwenye kiwango chake cha juu wakati akiwa na Real Madrid na pia Ufaransa."

Kiungo huyo wa zamani pia alizungumzia ushindi wa bao 1-0 walioupata Ufaransa mwishoni mwa wiki katika mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Finland, na kusema kwamba matokeo ndio kitu kikubwa cha kuzingatia.

"Kwa maoni yangu ilikuwa ni mechi nzuri kwa Ufaransa kwa sababu walitwaa pointi zote tatu. Kocha anahitaji muda zaidi ili kupata suluhu ya kila tatizo ndani ya kikosi chake."

No comments:

Post a Comment