Thursday, September 27, 2012

XAVI: ABIDAL ATARUDI KUICHEZEA BARCELONA NOVEMBA

Xavi (kushoto) akiwa na Abidal
BARCELONA, Hispania
Nyota wa Barcelona, Xavi amefichua kwamba Eric Abidal anaweza kurudi katika kikosi chao Novemba.

Beki huyo Mfaransa amekuwa nje ya kikosi cha Barca tangu April kufuatia iperesheni aliyofanyiwa ya kupandikiziwa ini, lakini alisema mwezi uliopita kwamba alikuwa na matumaini ya kuanza kucheza tena Desemba mwaka huu.

Mchezaji mwenzake wa Barcelona, Xavi sasa amesema kwamba Abidal anaweza kurudi kwenye kikosi chao Novemba, na amempongeza beki huyo mwenye miaka 33 kwa kujituma kwake ili kujiweka tena 'fiti' baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu.

"Anashangaza. Yeye ni mfano wa kuigwa," Xavi amesema leo.
"Sio tu kwamba yeye ni mchezaji nyota, amekuwa akijifua gym kila siku, asubuhi na jioni. Sisemi kwa uhakika kwamba atarudi Novemba, lakini ni kweli kwamba atarudi kati ya Novemba na Desemba."

Kiungo huyo mwenye miaka 32 alisifia kwa haraka kuwapo kwa Abidal katika kambi ya Barcelona, na anaamini kwamba anaonyesha mfano mzuri kwa wachezaji vijana ndani ya klabu yao.

"Anachangamsha chumba cha kuvalia, ni yeye anayefungulia muziki. Inaonekana kwamba sasa ana furaha zaidi kuwa nasi kuliko hata ilivyokuwa hapo kabla," Xavi amesema.

"Yeye ni mtu anayepaswa kubaki klabuni kama mfano kwa wachezaji vijana."

No comments:

Post a Comment