Friday, September 7, 2012

NANI ALITAKA MSHAHARA MKUBWA KULIKO HULK

Nani

MKURUGENZI Mtendaji wa Zenit St Petersburg, Maxim Mitrofanov amesema kiwango cha mshahara alichotaka winga wa Manchester United, Nani, ili kujiunga nao kilikuwa ni kikubwa mno hata kwao.

Zenit ilikamilisha uhamisho uliogharimu paundi milioni 100 kwa kuwasajili Hulk na Axel Witsel wiki iliyopita na wakajaribu kumsajili Nani jana.

"Kama Hulk alitaka mshahara wa euro 8 hadi euro milioni 10 kwa mwaka, matakwa haya hayakubaliki kwa Zenit," Mitrofanov alisema.

"Uhaisho wa Nani ulikwama kwa sababu hii, alitaka mshahara ambao hatuwezi kumlipa."

No comments:

Post a Comment