Tuesday, September 4, 2012

KIMOBITELI AREJEA EXTRA BONGO

Khadija Mnoga 'Kimobiteli' (kulia) akizungumza wakati akitambulishwa kurejea katika bendi ya Extra Bongo akitokea African Stars 'Twanga Pepeta' jijini Dar es Salaam leo. Picha: Sabato Kasika

MUIMBAJI nyota nchini Khadija Mnoga 'Kimobitel' amerejea katika katika mendi yake ya zamani ya Extra Bongo akitokea African Stars 'Twanga Pepeta'.

Kimobiteli alisema wakati wa kutambulishwa kwa wanahabari jijini Dar es Salaam leo kuwa amerejea katika bendi hiyo bila ya kushawishiwa na mtu na kwamba hakuwa na mkataba Twanga Pepeta.

Muimbaji huyo amewaahidi makubwa mashabiki wake na kwamba amerejea na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la 'Mgeni'.

Naye Mkurugenzi wa Extra, Ali Choki amesema kuwa Kimobitel ataimarisha kikusi chao ambacho kinahitaji sauti ya kike.

Choki amesema wanatarajia kumtambulisha muimbaji huyo katika maonyesho yao ya wiki ijayo kwani kwa sasa bado anaendelea na mazoezi na wenzake.

Alisema bendi yao itaendelea na maonyesho yao kama kawaida wiki hii ambapo kwa siku za Ijumaa na Jumapili hutumbuiza katika ukumbi wa White House-Kimara na Jumamosi Meeda Club, Sinza.

No comments:

Post a Comment