Friday, August 17, 2012

WENGER ASEMA HAKUWA NA JINSI ILA KUMUUZA RVP

Arsene Wenger
Arsene Wenger
Arsene Wenger


LONDON, England
MSHAMBULIAJI Robin Van Persie alitaka kuondoka Arsenal na akaiacha klabu hiyo ikiwa haina namna zaidi ya kumuuza, kocha Arsene Wenger amesema leo Ijumaa baada ya Mholanzi huyo kujiunga na Manchester United.

Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita, amesemaini mkataba wa miaka minne klabuni Old Trafford leo na kuhitimisha kipindi chake cha miaka nane cha kukaa Arsenal ambapo aliwafungia magoli 132 katika mechi 278.

"Tunahuzunika kumpoteza mchezaji bora tena kwa sababu moja rahisi - alibaki na mwaka mmoja tu katika mkataba wake. Alitaka kuondoka," Wenger ameuambia mkutano na wanahabari leo.

"Tulitarajia jambo hilo litatokea, hivyo tukawanunua Lukas Podolski na Olivier Giroud.

"(Kuwauzi wapinzani wetu) si jambo tulilolitaka lakini hapakuwa na chaguo jingine. Kulikuwa na klabu moja tu ambayo inamuhitaji kwa dhati katika kiwangoa mbacho tulidhani ni stahili na hao walikuwa ni Manchester United.

"Mwisho wa yote, hayo ndiyo maamuzi pekee ambayo tungeweza kufanya."

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kwamba dili hilo linathamani ya paundi milioni 24 na Wenger alisema Arsenal tayari "imeshawekeza pesa" kwa kuwasajili kiungo wa timu ya taifa ya Hispania, Santi Cazorla kutoka Malaga, winga wa timu ya taifa ya Ujerumani, Lukas Podolski kutoka FC Cologne na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Olivier Giroud kutoka kwa mabingwa wa Ligue 1, Montpellier.

"Kama itahitajika tutanunua wachezaji zaidi, lakini ukiangalia idadi ya wachezaji tulionao, tuna kikosi kikubwa. Tuna wachezaji ambao hawana hata nafasi ya kucheza kabisa.

"Kwa sasa naamini tunacho tunachohitaji kuwa na malengo na kucheza mchezo wetu."

Arsenal, iliyomaliza ya tatu katika ligi msimu uliopita - pointi 19 nyuma ya klabu za Manchester - itaanza kampeni mpya nyumbani Emirates dhidi ya Sunderland kesho Jumamosi saa 11:00 jioni.

Winga Alex Oxlade-Chamberlain (enka) na beki Laurent Koscielny (kiazi cha mguu) watakosa mechi hiyo lakini Theo Walcott, ambaye alitoka katika mechi ya kirafiki ya timu ya taifa ya England waliyoshinda dhidi ya Italia katikati ya wiki kutokana na maumivu ya paja, amepona.

Beki Thomas Vermaelen amepewa mikoba ya unahodha badala ya Van Persie.

No comments:

Post a Comment